Jifunze Njia Za Kukutana Na Wanawake Wapya
Kama wewe una aibu ya kukutana na wanawake ama unataka kuongeza ujuzi wako wa kukutana na wanawake wapya katika maisha yako basi hii post nimeitengeneza spesheli kwako. Njia hizi tulizoziorodhesha lazima uzifuatilie kwa umakini bila hivyo utajikuta pahali pabaya
Mbinu hizi zimefanyiwa utafiti na watu wengi sehemu tofauti tofauti na zimeonyesha manufaa makubwa kwa yeyote anayetumia. Hivyo wewe mahali popote pale ulipo usitie shaka na lolote lile. Manufaa ni ya kwako.
.
Mbinu hizi zimefanyiwa utafiti na watu wengi sehemu tofauti tofauti na zimeonyesha manufaa makubwa kwa yeyote anayetumia. Hivyo wewe mahali popote pale ulipo usitie shaka na lolote lile. Manufaa ni ya kwako.
.
Jinsi ya kukutana na wanawake wapya
1. Zifahamu sehemu nzuri za kukutana na wanawake
Sehemu za kujivinjari kama vilabu na baa ni sehemu nzuri za kukutana na wanawake lakini kama unataka mahusiano marefu na mwanamke basi sehemu hizo si nzuri kwako. Iwapo unataka mchepuko wa haraka basi unaweza kuenda kutafuta katika hizo sehemu.
Iwapo wewe ndio umeingia katika dunia ya kutongoza kwa sasa, basi ningekushauri utafute sehemu mbadala kwa sababu kutakufungua macho na ufahamu mpango mzima kuhusiana na maswala ya mahusiano na mapenzi. Sehemu nzuri za kukutana na wanawake ni:
- Supermarket
- Mkahawa
- Bustani
- Vituo vya mabasi
- Chuoni
2. Jaribu mitandao ya kutafuta wachumba, wapenzi
Hii inaweza kuonekana kama utata kwako lakini kulingana na utafiti ni kuwa wanaume wengi hupata wachumba wao kupitia mitandao ya kutafuta wachumba. Uzuri wa mitandao hii ni kuwa haina stress ya kujisumbua kuzunguka, unatafuta mchumba ukiwa nyumbani kwako ukiwa umetulia. Pia mitandao hii inakupa fursa ya kupata mchumba ambaye mnagawa maslahi na tabia moja.
3.Usishushe hadhi yako
Iwapo unataka kutongoza mwanamke sehemu yeyote ile, usijaribu kushusha hadhi yako. Iwapo unaamini ya kuwa wewe ni mzuri zaidi kwa mwanamke basi pia yeye ataamini hivyo hivyo. Pia iwapo unaona hauna uwezo wa kumvutia mwanamke, elewa ya kuwa vivyo hivyo wanawake watakuona kama mwanaume usiyejiamini ambaye huna confidence ya kuwaaproach ama kuwatongoza.
Wanawake hupenda wanaume ambao wana confidence na wanaopenda kuchukua misimamo ya haraka.
4. Kuwa na mipango
Kama iwapo unataka kukutana na mwanamke mara ya kwanza ama wakati mwingine, hakikisha ya kuwa unaweka mpango unaoeleweka ili usipate tatizo mbeleni. Mfano unamtoa out mwanamke, hakikisha ya kuwa unaifahamu vyema sehemu unapanga kumtoa out ili usianze kupapatika kuhusu wapi na nini la kufanya wakati mmetoka sehemu hizo.
Wanawake hupenda wanaume ambao huwa na mwongozo wa mambo ambayo hufanya.
Sehemu nzuri za kukutana na mwanamke ni katika mkahawa, gym, na baa. Hakikisha ya kuwa sehemu unayoichagua inapendeza.
5. Uwe unapendeza kila wakati
Iwapo unataka kuwa na mahusiano mazuri na wanawake basi unafaa uwe unapendeza kimuonekano. Hakikisha ya kuwa unauboresha mwonekano wako na pia umaintain kila wakati. Kuvalia nguo nzuri mara kwa mara ni muhimu lakini usivuke mipaka. Ni muhimu kufanya hivi kwa sababu huwezi kujua lini ama wapi unaweza ukakutana na mwanamke utakaye mzimia.
6. Fanya mazoezi ya ujamiifu wako
Ujamiifu ni socialization na wengine. Iwapo unataka kukutana na wanawake wengi katika maisha yako, basi kigezo cha kujamiiana na wengine ni muhimu. Kutembea sehemu za vilabu, baa, sehemu ambazo kuna matukio flani ni muhimu ili kunoa kipawa chako cha kutangamana na wengine.
Tumia fujo wakati ambapo unatangamana na wanawake ili uboreshe ubabe wako. Kama ni kuenda kwa kilabu, hakikisha ya kuwa unadensi na wanawake tofauti tofauti. Hii inakupa confidence kwa mwanamke.
Pia hakikisha ya kuwa unaenda wakati ufaao sehemu kama hizi. Mfano nenda kwa klabu wakati watu wamekuwa wengi. Pia usijifiche wala kuogopa yeyote yule.
7. Usibabaikie kutemwa
Kila mtu katika maisha yake ashapitia wakati flani ambapo amekataliwa na mtu flani, so kukataliwa ni jambo la kawaida na halifai kusumbua mtu akili. Kando na hivyo, kukataliwa hakumaanishi ya kuwa unafanya makosa. Wakati mwingine huwa ni kuwa wanawake wengine hawataki kuwa katika mahusiano, washachumbiwa ama sababu nyingine kama hizi.
Kumalizia ni kuwa kuna mbinu tofauti tofauti na sehemu tofati za kutafuta mchumba hivyo woga la kutemwa halifai kuwa swala kuu.
Kumalizia ni kuwa kuna mbinu tofauti tofauti na sehemu tofati za kutafuta mchumba hivyo woga la kutemwa halifai kuwa swala kuu.
8. Pata ujuzi kutoka kwa wanaume wengine
Ukweli usemwe, hakuna mwanaume hapa duniani yuko sawa asilimia 100. Hivyo ni vizuri kupata ujuzi kwa kuwauliza wenzako ni vipi waliweza kutongoza ama kupata windo fulani.
Ingawa ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa marafiki zako, mimi naona ushauri wa mtu huwa tofauti na mwingine hivyo mara nyingi ushauri kutoka kwa mwanaume mwingine unaweza kukupotosha ama kuegemea upande mmoja.
Ukweli usemwe, hakuna mwanaume hapa duniani yuko sawa asilimia 100. Hivyo ni vizuri kupata ujuzi kwa kuwauliza wenzako ni vipi waliweza kutongoza ama kupata windo fulani.
Ingawa ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa marafiki zako, mimi naona ushauri wa mtu huwa tofauti na mwingine hivyo mara nyingi ushauri kutoka kwa mwanaume mwingine unaweza kukupotosha ama kuegemea upande mmoja.
Post a Comment