Ishara 10 Kuonyesha Rafiki Yako Anamtamani Girlfriend Wako Kimapenzi
Hebu fikiria jambo hili: Kwa muda wa miezi miwili umekuwa ukimfukuzia huyu mwanamke. Umetumia kila mbinu unazozijua za kutongoza. Umeuliza marafiki zako wakusaidie kukupa ushauri jinsi ya kumnasa huyu mwanamke. Halafu baadaye huyu mwanamke ameonyesha dalili za kukupenda. Ukaanza kumtuza kwa kumrushia pesa mara kwa mara (kitendo tunachokipiga vita hapa Nesi Mapenzi) ili akupende. Na baada ya kukudondoa hela za kutosha huyu mwanamke akakupenda. Mkaanza kuishi vizuri kama wapenzi. Lakini kabla hujatulia kidogo ukashtukizia rafiki yako wa karibu/dhati amemzuzua mpenzi wako na kukupokonya.
Umeachwa bila kujua wala kuona ishara zozote. Unaanza kujilaumu na kujiuliza maswali ni kitendo gani ulichofanya mpaka rafiki yako akakupokonya mpenzi wako. Unamlaani mpenzi wako kwa kukuacha. Unaanza kuingiwa na misongo ya mawazo isiyoisha. Unapiga hesabu miezi uliyoipoteza kumfukuzia mwanamke ambaye kumbe atakuja kupokonywa na rafiki yako. Mbaya zaidi unahisabu hasara ulizozipitia kumpata huyu mwanamke. Pesa zote alizokunyanyasa. Mbaya zaidi labda hata hajakupa nafasi ya kulionja tunda lake.
Well, haya ni masaibu yaliyomtokea Joni (jina lake la kweli tumelibana ili kumstiri) ambayo alituelezea hapa Nesi Mapenzi kupitia email yetu. Hivi ndivyo alivyoandika.
Well, hii ni changamoto ambayo inaendelea kuwakumba wanaume nyanjani. Na leo tumeamua kumsaidia Joni, na yeyote yule ambaye yuko katika hatari ya kuwa kama Joni. Tumekuja na mbinu za kutambua iwapo rafiki yako anammezea mate mpenzi wako.
Hapa Nesi Mapenzi hatungependa kuona juhudi zetu za kuwafunza watu kutongoza zikiharibiwa na mafisi wachache ambao lengo lao ni kuwavunjia uhusiano wengine.
Hapa Nesi Mapenzi hatungependa kuona juhudi zetu za kuwafunza watu kutongoza zikiharibiwa na mafisi wachache ambao lengo lao ni kuwavunjia uhusiano wengine.
Zama sisi!
Ishara #1. Unahisi uwepo wake. Ok. Huyu rafiki yako ni yule wa dhati. Mnaweza kukaa hata miezi sita bila kuwasiliana kwa simu ama popote vile lakini ile siku ambayo mtakutana ni kama ambaye mlionana siku ya jana. Yaani mnaongea na kujifurahisha kana kwamba miezi sita bila kuwasiliana ni kama siku moja au mbili.
Lakini ghafla baada ya kumtambulisha kwa mpenzi wako unashangaa kuona huyu rafiki yako anawasiliana na wewe mara kwa mara. Haipiti siku moja au mbili anawasiliana nawe. Haikuwa uraibu wake kuwasiana na wewe lakini tangu umtambulishe kwa mpenzi wako amekuwa anawasiliana na wewe siku baada ya siku. Hapa jitahadhari sana. Ameshamuona mpenzi wako na anaanza mawindo yake. Unachohitajika kufanya ni kumuonya na mapema kuhusu hii tabia mpya.
Ishara #2. Si mcheshi. Huyu rafiki yako huwa hapendi kucheka. Huwa mara nyingi anajizuia kucheka. Hata kuwe na kitu ambacho kinachekesha kiasi gani yeye atatabasamu tu na kujipa shughli.
Ghafla kukutana na girlfriend wako mambo yamebadilika. Kitu chochote cha utani kitakachotoka kinywani mwa yeyote atakuwa wa kwanza kucheka kwa nguvu. Na mara nyingine atajichekea bila sababu. Hapa usidanganywe ukaona kuwa amekuwa na kichaa, la. Anapiga hesabu zake. Anajaribu kumwonyesha mpenzi wako kuwa yeye ni mtu friendly na yeyote anaweza kuongea na yeye. Anajaribu kujitokeza kama mwanaume ambaye si mgumu. Hapa jitahadhari sana.
Ishara #3. Yuko upande upi? Umetoka out kwenda kula bata ama kitu kingine kama hicho, halafu kwa bahati nzuri au mbaya girlfriend wako na rafiki yako wamekutana, na mazungumzo yakashika kasi. Je umegundua kuwa kila kitu ambacho mpenzi wako akisema huyu rafiki yako anakubaliana nacho?
Halafu mbaya zaidi ni kuwa kila kitu utakachosema anakipinga na anakubaliana na mitazamo ya girlfriend wako. Kama anaweza kuwa mpole na kukubaliana na mtu ambaye hamjui vizuri na kumpinga rafiki ambaye wamekuwa pamoja miaka mingi basi hapo lazima utie shaka. Kuna kitu analenga.
Ishara #4. Mtindo chenga. Rafiki yako ni mtu wa miraba minane. Muda mwingi yeye huvalia nguo za kuonyesha mwili wake. Huonyesha maungo. Yaani amezoea tu kuvalia kikawaida. Hakuna siku utawahi kumwona amevalia nguo za kiofisi ama kuvalia shati lisilokuwa na nembo.
Mara ghalfa unamwona ametokezea bila kualikwa akiwa amevalia kama Jason Stratham wa Transporter ama amevalia kama James Bond vile. Hapa jambo la kwanza ambalo unapaswa kuzingatia ni kuwa kuna tatizo flani. Si kuwa ameamua kubadilika bali analenga kumzuzua mpenzi wako.
Ishara #5. Amemtema wake. Huyu rafiki yako ana mpenzi. Mpenzi wake wa dhati wamekuwa pamoja kwa muda na anaonyesha kumpenda mpenzi wake. Yeye na mpenzi wake ni vigumu kuachana na kila siku anamwongelea. Halafu siku moja amekutana na mpenzi wako, na ile ya pili anayokutana na wewe anakwambia kuwa yuko single.
Ameachana na mpenzi wake wa maisha, na zaidi ni kuwa hatoa sababu za maana kwa nini ameachana naye. Hapa hakuna kesi. Amefall na girlfriend wako. Na amejiweka katika hali ya kuwa anaweza kumwaproach mpenzi wako bila tashwishi.
Ishara #6. Genteli. Huyu jamaa, anajulikana kuwa ni domo zege. Maneno yoyote atakayomtamkia mwanamke ni kama matope. Mwanamke yeyote akiongea nayeye anamkataa. Mara ghafla mnashtuka amekuwa gental. Amekuwa anaongea na sauti ya utulivu iliyopangwa. Huyu lazima umweke katika ramani yako ya uchunguzi.
Ishara #7. Anapuliza miski kwa hewa. Huyu ni jamaa ambaye hapaki marashi yeyote. Yale marashi ya mwisho anayakumbuka ni yale yanauzwa kwa vipimo pale sokoni rejareja. Lakini kidogo kidogo unaona anaaza kujipaka marashi ya Nivea ama latest scents za Axe kila wakati mpenzi wako anapokuwa karibu. Hii ni dalili ya kutosha unapaswa kuizingatia.
Ishara #8. Kutoka beta. Mtu ambaye amekuwa upande wako tangu jadi. Lakini ghafla huyu rafiki yako anakujeukia pindi mpenzi wako anapokuwa karibu. Anafanya juu chini kuhakikisha anakuangusha. Kila kitu anatoa sababu za kukupinga ama kuonyesha haufai. Anajitokeza kama mwanaume alpha. Hakuna kitu kitamzuia mbele yake.
Ishara #9. Umepata jumbe. Katika mazingira yasiyoeleweka, huyu mwanaume ameweza kupata namba ya mpenzi wako, labda aliipata kwa njia ya kualikwa kwa birthday party ama kwa njia nyingine, lakini anaanza kumtumia mpenzi wako meseji zisizokuwa na misingi mchana na usiku kutwa. Kama girlfriend wako atajitokeza bila hatia na kukuonyesha hizo jumbe basi mara moja unapaswa kumfukuza huyu rafiki yako kutoka kwa maisha yako ama atakuaibisha kama vile Joni alivyoaibika.
Ishara #10. Ni zawadi. Si kila mtu anaweza kutumia mbinu fioa kumtongoza mwanamke kama tumeorodhesha awali, na huyu rafiki yako anaweza kuamua liwe na liwalo na kujaribu kumzuzua mpenzi wako. So, kama utamwona anakuja kwako akiwa amebeba zawadi kubwa kubwa na maboksi ya chokoleti ghali kumletea girlfriend wako basi wakati umefika kumpa neno lako.
Kama unataka mpenzi wako akuteme mara moja aende kwa rafiki yako, basi baada ya kusoma ishara hizi na umegundua kuwa 6 kati ya hizi 10 rafiki yako anakufanyia, wewe zubaa. Bora tu usije ukalalamika kama Joni. Upo!? Mafanikio kwako.
Post a Comment